• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka jumuiya ya kimataifa ihimize mchakato wa ukuaji endelevu wa miji

    (GMT+08:00) 2017-09-06 19:10:47

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema China inaitaka jumuiya ya kimataifa ishirikiane kuunda umoja wa jaala ya binadamu wote, kuhimiza mchakato wa ukuaji endelevu wa miji inayowapatanisha watu wote, kuboresha mazingira ya makazi ya binadamu na kujenga dunia nzuri ya binadamu

    Balozi Wu amesema hayo jana alipohutubia mkutano wa 71 wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ajenda ya miji mipya. Amesema ajenda hiyo inaonesha mwelekeo wa maendeleo ya miji duniani katika siku za baadaye. Pia inahakikisha jumuiya ya kimataifa inachukua njia ya ukuaji endelevu wa miji ambayo inazingatia zaidi mahitaji ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako