• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti wa benki ya Stanbic unaonesha kuwa uchaguzi umeathiri biashara Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-06 20:26:07

    Hali ya biashara nchini Kenya imeshuka mwezi uliopita kutokana na wasiwasi kuhusu uchaguzi Mkuu.

    Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa Benki ya Stanbic wa usimamizi wa uuzaji na ununuaji.

    Utafiti huo unaonesha kuwa hali hiyo huenda ikaendelea baada ya Mahakama ya juu kufuta uchaguzi wa urais.

    Shughuli za sekta binafsi zimepungua hadi alama 42.0 mwezi Agosti kutoka alama 48.1 mwezi Julai.

    Kushuka huku kwa jumla kumesababishwa na kuanguka kwa shughuli za biashara.

    Utafiti huo umeonyesha kuwa usambazaji mdogo wa fedha na hali hafifu za uhitaji kama sababu kuu za kushuka kwa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako