• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na China zafanya utafiti wa pamoja kuongeza uzalishaji

    (GMT+08:00) 2017-09-06 20:26:47

    Wataalamu kutoka chuo cha sayansi cha China- Chinese Academy of Sciences (CAS) wametia saini mkataba mpya baina yao na watafiti wa Rwanda kusaidia kuongeza uzalishaji wa kilimo kupitia uhifadhi wa mazingira ulioboreshwa.

    Kulingana na mkataba huo,watafiti wa China wataungana na wenzao katika chuo kikuu cha Lay Adventists cha Kigali (UNILAK), kufanya utafiti kuhusu jinsi Rwanda inaweza kulinda mazingira ya kilimo dhidi ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

    Naibu Kansela wa chuo cha UNILAK Dkt Jean Ngamije amesema utafiti huu wa pamoja wa uhifadhi wa maji na mchanga umeundwa kuisadia Rwanda kuboresha uwezo wa uzalishaji na kuongeza utoshelevu wa chakula.

    Matokeo ya utafiti huu wa miaka mitano yanatarajiwa kutoa ushahidi wa kisayansi,usaidizi wa teknolojia na miradi ya maonyesho ili kuboresha hali za maisha kwa kujenga ustahimilivu wa hali ya hewa na kurejesha na kuhifadhi mazingira muhimu katika nchi zinazoendelea.

    Kulingana na Dkt Li Fadong,mtafiti kutoka taasisi ya sayansi ya kjiografia na rasilimali za asili katika Chuo cha Sayansi cha China,China na Rwanda zitabadilishana uzoefu na utaalamu ili kushughulikia changamoto hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako