• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wayne Rooney matatani kwa kuendesha akiwa amelewa

  (GMT+08:00) 2017-09-07 08:27:12

  Kocha wa club ya Everton ya England Ronald Koeman jana ameripotiwa kumuita nahodha wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England anayeichezea Everton kwa sasa Wayne Rooney na kuongea nae kuhusu tuhuma zinazomkabili za kuendesha gari akiwa amelewa. Rooney anatuhumiwa na Polisi wa Cheshire baada ya kukamatwa usiku wa Ijumaa ya August 31 2017 akiwa anaendesha gari akiwa amelewa, kitu ambacho ni kinyume na sharia. Baada ya kukamatwa Rooney aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa mahakamani September 18 2017. Nyota huyo wa zamani wa Man United kama akikutwa na hatia kwa kosa hilo club ya Everton itamkata mshahara wa wiki mbili unaokadiriwa kufikia pound 320,000, Rooney hata hivyo amepewa onyo baada ya kuzungumza kwa muda mrefu na kocha Ronald na kuambiwa kama anataka kudumu katika club hyo inabidi abadilike.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako