• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pius Buswita atoka kitanzini baada ya kukubali kuilipa Kalabu ya Simba

  (GMT+08:00) 2017-09-07 08:27:35

  Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za wachezaji imesema haioni haja ya kuendelea kumfungia kiungo aliyesaini mkataba katika vilabu viwili tofauti Pius Buswita baada ya yeye kukubali kuilipa Simba Milioni 10. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Elias Mwanjala baada ya vilabu hivyo kukaa pamoja na kuafikiana juu ya mchezaji huyo.

  Hata hivyo, Kamati hiyo imesema lengo hasa la kuridhia kumtoa kifungoni Pius ni kutokana na kuona mpira ndiyo ajira yake ambayo anaitegemea. Kwa upande mwingine, Klabu ya Simba wamedai walipwe pesa ya nauli ya ndege waliyomlipia mchezaji huyo endapo watamchukua ambapo Yanga wamekubali kuilipa pesa hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako