• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa FOCAC kuhusu upunguzaji umaskini na maendeleo wafanyika Mauritius

    (GMT+08:00) 2017-09-07 09:37:04

    Mkutano kuhusu maendeleo na upunguzaji wa umaskini wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC umefunguliwa jana mjini Balaclava, Mauritius, ambapo washiriki wamejadili ushirikiano wa China na Afrika kwenye kukabiliana na changamoto mpya za kupunguza umaskini.

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, waziri mkuu wa Mauritius Bw Pravind Kumar Jugnauth amesema njia mwafaka ya kutatua suala la umaskini ni kuwawezesha familia maskini zijitoe kwenye umaskini na kujikimu kimaisha.

    Mjumbe wa China kwenye mkutano huo Bw Xia Gengsheng amesema pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" limechangia ufumbuzi wa China katika kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kuhimiza maendeleo ya pamoja. Amesema China itahimiza utekelezaji wa mipango kumi ya ushirikiano kati ya China na Afrika, pamoja na Ajenda ya mwaka 2063 kwa Afrika, ili kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, kuongeza nafasi za ajira, kuondoa umaskini, na kupata ukuaji shirikishi wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako