• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2017-09-07 09:50:40

  Rais Xi Jinping wa China jana aliongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Donald Trump.

  Katika mazungumzo hayo, Rais Xi ameeleza kuwa hivi sasa mawasiliano na ushirikiano kati China na Marekani katika sekta mbalimbali zinaendelea kwa hatua madhubuti, ambapo pande hizo mbili zinaandaa duru ya kwanza ya mazungumzo kuhusu jamii na utamaduni, na mazungumzo kuhusu utekelezaji wa sheria na usalama wa mtandao wa Internet.

  Rais Trump amesema kudumisha mawasiliano ya karibu kati yake na Rais Xi na kuimarisha uratibu katika masuala muhimu ya kimataifa na ya kikanda kuna umuhimu mkubwa.

  Wakizungumzia suala la Peninsula ya Korea, rais Xi amesisitiza kuwa China itafanya juhudi bila kusita katika kutimiza lengo la Peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, na kulinda utaratibu wa kutoeneza silaha za nyuklia duniani. Kwa upande wake, Rais Trump amesema, Marekani inapenda kuimarisha mawasiliano kati yake na China ili kupata ufumbuzi wa suala hilo mapema iwezekanavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako