• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya Ulaya yaamua kuwa mpango wa uhamisho wa wakimbizi ni halali

    (GMT+08:00) 2017-09-07 09:57:34

    Mahakama ya Ulaya jana imetoa hukumu na kuunga mkono mpango wa uhamisho wa wakimbizi uliopitishwa miaka miwili iliyopita, ambao umefuta pingamizi la serikali za Hungary and Slovakia.

    Serikali za nchi hizo mbili zimesema mpango huo haukupitishwa na nchi wanachama wote wa Umoja wa Ulaya, kwa hivyo mchakato huo sio halali. Kutokana na pingamizi hilo, mahakama ya Ulaya imetoa hukumu kuwa, mpango huo sio sheria, hauna haja ya kupitishwa na mabunge ya nchi wanachama wa Umoja huo, pia hauna haja ya kupitishwa na baraza la Umoja wa Ulaya.

    Nalo Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limepongeza uamuzi huo na kusema, uamuzi huo unatoa ishara ya kusisitiza umuhimu wa mshikamano na uwajibikaji wa pamoja kati ya nchi wananchama wa Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako