• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakubali Umoja wa Mataifa kuchukua hatua zaidi kuhusu suala la peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-09-07 19:19:14

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, kufuatia mabadiliko mapya yaliyotokea katika peninsula ya Korea, China inaridhia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za lazima.

    Bw. Wang amesema hayo akifanya mazungumzo na naibu waziri mkuu wa Nepal na kukutana na waandishi wa habari kwa pamoja. Amesema, Korea Kaskazini inatakiwa kuacha kushikilia msimamo wake, na kupuuza maoni ya pamoja na mstari wa mwisho wa jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Wang amesisitiza kuwa China inashikilia msimamo wa kutatua suala la Korea Kaskazini kwa njia ya mazungumzo, huku akisema vikwazo ni nusu ya ufunguo wa kutatua suala hilo, na nusu nyingine ni mazungumzo. Hivyo, hatua yoyote mpya itakayochukuliwa na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuwa msingi wa kuizuia nchi hiyo kuendeleza teknolojia ya nyuklia na kusaidia kuhimiza kuanzisha tena mazungumzo haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako