• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yawawekea vikwazo maofisa watatu wa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-09-07 19:21:17

    Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo maofisa wawili waandamizi wa serikali ya Sudan Kusini na aliyekuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo kutokana na kuhusika na vita ya wenyewe kwa wenye nchini humo.

    Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kuwa mali zote zilizoko nchini Marekani za waziri wa habari wa Sudan Kusini Bw. Michael Makuei Leuth, makamu mkuu wa jeshi Bw. Malek Reuben na mkuu wa majeshi aliyefutwa kazi Bw. Paul Malong zimezuiliwa, na maofisa hao wamepigwa marufuku kuingia Marekani, serikali ya Marekani pia imeziwekea vikwazo kampuni tatu zinazomilikiwa au kudhibitiwa na mmoja wa maofisa hao.

    Vikwazo hivyo vimekuja siku chache baada ya ofisa wa serikali ya Marekani kusema serikali ya Marekani inafikiria kupitia upya msaada wake kwa Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako