• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Treni mpya nchini Kenya yatimiza siku 100

    (GMT+08:00) 2017-09-08 08:29:57

    Zimetimia siku mia moja tangu treni ya kisasa ya SGR nchini Kenya ianze kusafirisha abiria. Shirika la reli mpya limelazimika kuongeza idadi ya mabehewa ili kukidhi mahitaji ya kuongezeka kwa idadi ya abiria. Matunda ya huduma za treni hiyo mpya yameanza kuonekana, ikiwa ni pamoja na kushamiri kwa biashara za kando ya reli.

    Abiria wanaosafiri kwa kutumia reli hiyo wanafurahia kupungua kwa muda wa kusafiri, wakati hapo awali iliwachukua muda wa saa 10 kwa kutumia barabara, lakini sasa wanaweza kufanya biashara kwa haraka kwani muda wa usafiri umepungua. Mbali na kupungua kwa muda wa kusafiri, watumiaji wa reli hiyo pia wamefurahia gharama za chini za usafiri, kwani sasa nauli ni shilingi mia saba za Kenya.

    .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako