• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • David Haye amini pambano lake dhidi ya Anthony Joshua kuwa la kipekee

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:49:17

  Bondia raia wa Uingereza, David Haye anaamini pambano lake dhidi ya Anthony Joshua litakuwa kubwa na la kipekee ambalo halijawahi tokea katika ardhi ya nchi hiyo. Haye, anahitaji kucheza na Anthony Joshua hapo mwakani katika pambano ambalo anaamini litakuwa kubwa halijawahi kutokea nchini Uingereza hii ni mara baada ya kurudi katika ulingo.

  Bondia huyo wa uzito wa juu anatarajia kurejea tena ulingoni mwaka huu baada ya kupona majeraha aliyo yapata wakati wa pambano lake dhidi Tony Bellew mwezi Machi Makubaliano yanaendelea kwaajili ya mchezo wa marudiano kati ya bondia huyo dhidi ya Bellew pambano linalotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu ili kujiweka sawa kwaajili ya pambano lake na Joshua 2018.

  David Haye mwenye umri wa miaka 36, ameongeza kuwa anahitaji mapambano manne makubwa ndipo amini kuwa anaweza kupambana na mtu sahihi bondia namba moja kwake, Anthony Joshua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako