• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wachezaji wa Brazil waziwakilisha vyema timu zao michuano ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:50:03
  Wachezaji wa ligi kuu nchini Hispania La Liga kama ilivyokuwa ligi nyingine walisafiri kwenda kuziwakilisha timu zao za taifa katika michuano ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.

  Wachezaji wengi wa Brazil waliziwakilisha vyema timu zao na kushinda michezo yote miwili waliyozichezea timu za taifa lakini kwa Wacrotia Modric na Kovacic mambo yalikuwa tofauti. Cristiano Ronaldo alipiga hat trick wakati akiibeba Ureno dhidi ya Faroe Islands lakini katika mchezo wa pili Ureno waliibuka kidedea kwa bao 1 kwa nunge ila Ronaldo hakufunga katika mchezo huo. Wales ambao waliongozwa na Gareth Bale waliibuka kidedea katika michezo yao miwili wa kwanza dhidi ya Austria wakashinda bao 1 kwa nunge na kisha mchezo wa pili wakaibuka kidedea kwa bao 2. Marcelo na Cassemiro waliisaidia Brazil kuifunga Ecuador kwa mabao 2 kwa 0 lakini katika mchezo uliofuata kati ya Brazil na Colombia nyota hao waliwekwa pembeni. Isco, Sergio Ramos, Marco Asensio, Lucas Vasquez walikuwepo katika timu ya taifa ya Hispania ambayo iliifunga Italia bao 3 na kisha wakaipiga bila huruma timu ya taifa ya Liechtestein mabao 8 kwa 0. Lakini kwa upande wa nyota wawili wa timu ya taifa ya Croatia Luca Modric na Kovacic hali ilikuwa si hali kwani baada ya kuipiga timu ya taifa ya Kosovo kwa bao 1 kwa nunge walikubali kufungwa bao 1 kwa 0 na Uturuki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako