• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rodger Federer nje ya muchuano ya wazi ya Marekani

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:56:02

  Katika kitu ambacho mashabiki wengi wa mchezo wa tennis walikuwa wakikisubiria kwa hamu ilikuwa kuwaona wababe wawili wa mchezo huo Rafael Nadal na Rodger Federer kukutana katika Michuano ya wazi ya Marekani.

  Lakini Juan Martin Del Potro amekatisha ndoto hiyo ya wapenzi wa tennis baada ya kumfunga na kumuondoa Rodger Federer kwa kumpiga seti 7-5,3-6,7-6 na 6-4 katika mchezo ambao Federer alipewa nafasi kubwa kuibuka kidedea.

  Kama Federer angeshinda mchezo huu dhidi ya Martin Del Potro basi angeenda kupambana na Nadal lakini tofauti na matamanio ya wengi sasa Del Potro ndio anakwenda kukutana na Rafael Nadal.

  Del Potro anaonekana kuwa kizuizi kikubwa kwa wafalme hawa kukutana kwani miaka minane iliyopita alimtoa Nadal katika mashindano haya na kisha akaenda katika fainali na kumfunga Rodger Federer.

  Kwa matokeo haya sasa Del Potro atakutana na Rafael Nadal Ijumaa katika fainali ya michuano hii huku Nadal akipewa nafasi kubwa kulipiza kisasi kwa Potro kwa matokeo yaliyotokea miaka 8 iliyopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako