• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wenger amzungumzia Sanchez na ajipa moyo kuhusu ubingwa

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:56:22

  Katika kipindi cha usajili suala la Alexis Sanchez lilitawala sana vichwa vya habari lakini habari njema ni kwamba Arsenal walifanikiwa kupambana na Alexis Sanchez na amebaki katika timu yao.

  Kocha Arsene Wenger amesema kubaki kwa Sanchez ilikuwa jambo muhimu sana kwao japokuwa dirisha la usajili halikuwa zuri sana kwao lakini ana imani kubwa Sanchez atakuwa katika kiwango kizuri na atawasaidia sana. Wenger amesema Sanchez atarudi katika kiwango chake kikubwa mapema sana. Kuhusu kiwango cha timu Wenger amesema ni mechi tatu tu zimechezwa na matokeo yaliyotokea hana furaha nayo lakini safari bado ni ndefu na anaweza kupambana na kubeba ubingwa wa Epl kwani bado michezo 35 na viwango vya wachezaji vinabadilika muda wowote hivyo wanaweza kuwa vizuri sana na chochote kitatokea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako