• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Tanzania ajiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi wa madini

    (GMT+08:00) 2017-09-08 09:32:36

    Waziri wa nchi, ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa wa Tanzania Bw George Simbachawene amejiuzulu wadhifa wake, na kusema hana kinyongo na anaheshimu agizo la rais John Magufuli kuhusu waliotajwa kwenye ripoti mbili kuhusu ufisadi kwenye sekta ya madini alizopokea jana.

    Bw Simbachawene amesema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa ajili ya kulinda sifa ya serikali ya Tanzania. Amesema yeye hahusiki na ufisadi, lakini ameamua kujiuzulu ili kupisha uchunguzi zaidi.

    Rais Magufuli jana alipokea ripoti mbili kuhusu uchunguzi wa tuhuma za ufisadi na ukwepaji kodi kwenye sekta ya biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako