• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamanda wa jeshi la Libya hatahudhuria Mkutano wa Afrika kuhusu suala la Libya

    (GMT+08:00) 2017-09-08 09:39:23

    Kamanda wa jeshi la eneo la mashariki la Libya meja jenerali Khalifa Haftar amesema hatahudhuria Mkutano wa viongozi wa Afrika kuhusu mgogoro wa Libya utakaofanyika Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo.

    Mkuu wa ofisi ya habari ya jeshi la Libya Bw. Khalifa Obeidi ameliambia shirika la habari la Libya kuwa, meja jenerali Khalifa Haftar ameomba udhuru kwa kutoshiriki katika mkutano huu, lakini hakutaja sababu halisi.

    Mkutano huo utakaoendeshwa na Kongo Brazzaville unalenga kuondoa hali ya mvutano inayokwamisha utekelezaji makubaliano ya amani ya Libya yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, na kuhimiza maafikiano ya kitaifa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako