• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Ufaransa

    (GMT+08:00) 2017-09-08 19:36:38

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa njia ya simu.

    Rais Xi amesema, mkutano wake wa kwanza na rais Macron huko Hamburg ulifikia makubaliano muhimu kuhusu kuendeleza uhusiano wenye nguvu wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili. Amesema pande mbili zinatakiwa kuendelea kufanya ushirikiano ili kutimiza kiwango cha juu cha kunufaishana na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano huo.

    Rais Macron ameipongeza China kwa kufanikiwa kufanya mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS huko Xiamen, huku akisema kuwa Ufaransa na China ni wenzi wa kimkakati wa pande zote. Pia amesema, katika hali ya sasa ya kimataifa, nchi hizo mbili zinatakiwa kushirkiana zaidi katika kukabiliana na changamoto ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako