• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar-Mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali Kisiwani Zanzibar umepanda kwa asilimia 1.4, kutoka 4.1 kuanzia mwezi Julai hadi asilimia 5.5 katika mwezi Agosti mwaka huu.

  (GMT+08:00) 2017-09-08 19:52:19

  Kupanda kwa mfumko huo kumetokana na kuagizwa kwa bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi sambamba na ongezeko la bei katika soko la dunia. Akizunguymza na radio China Kimataifa, ofisa Mtakwimu serikalini Kisiwani humo, Salma Saleh Ali amesema kuwa bei za bidhaa zimeongezeka kwa asilimia 1.4.

  Ameongeza kuwa katika mwezi wa Agosti 2017, bidhaa za chakula na zisizo za chakula zilipanda kwa asilimi 6.1 ikilinganishwa na mwezi wa Julai ambapo ilikuwa ni asilimia 2.7.

  Hata hivyo ameongeza kuwa kwa ujumla mfumko wa bei kwa mwaka kutoka Agosti ya mwaka 2016 umepanda hadi kufikia 105.2 kutoka 99.6 ya Agosti mwaka 2017. Pia ameeleza kuwa mchele wa Mapembe umefikia asilimia 5.1, huku mchele wa Mbeya ukiwa asilimia 3.4, Jasmini asilimia 3.0, Basmati asilimia 1.9, Unga wa Mahindi asilimia 12.4. Sukari katika mwezi huu imepanda kwa asilimia 10.2 na Mafuta ya Taa 1.7, Petroli 1.5. Mkuu wa Idara ya Kiuchumi za Takwimu Abdul Ramadhan amesema kuwa ili hali ya mfumko wa bei isijitokeze tena ni lazima watu wajenge tabia ya kutumia vyakula zaidi wanavyozalisha wenyewe pamoja na kurejeshwa utaratibu wa kuweka akiba katika maghala yao ya chakula ili viweze kutumika endapo kutakuwa na upungufu wa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako