• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nairobi-Chama cha wafanya biashara nchini Kenya kimesema nchi hiyo imepoteza mabilioni ya fedha kutokana na msukosuko wa kisiasa unaoshuhudiwa hivi sasa.

  (GMT+08:00) 2017-09-08 20:55:33
  Chama hicho kimesema uchumi wa nchi hiyo umepoteza jumla ya shilingi bilioni 21.3 tangu mahakama ya juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wiki iliyopita. Mwenyekiti wa chama hicho Kiprono Kitonny amesema wawekezaji wengi wanaogopa kuwekeza kwa kuhofia mambo huenda yakawa mabaya. Ameongeza kuwa nafasi za kibiashara pia zimepungua huku sekta ya kibinafsi ikiathirika pakubwa. Kitonny amewataka wanasiasa kuheshimu uamuzi wa mahakama na kutoingilia shughuli za tume huru ya uchaguzi nchini Kenya. Amesema ikiwa hilo litatendeka basi wawekezaji watajenga imani ya kuwekeza fedha zao kwa urahisi.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako