• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya makaburi 110 ya halaiki yaligundulika katikati mwa Burundi.

    (GMT+08:00) 2017-09-09 18:20:52

    Tume ya ukweli na usuluhishi ya Burundi(TRC) imesema imegundua zaidi ya makaburi 110 ya halaiki katika jimbo la Mwaro lililopo katikati ya nchi hiyo. Mwenyekiti wa tume hiyo bwana Jean Louis Nahimana amesema kuwa zaidi ya makaburi 110 ya watu waliouawa kwenye mauaji ya halaiki yaliyotokea kati ya mwaka 1972 na 1993 yaligunduliwa kwenye maeneo tofauti ya jimbo hilo.

    Nahimana alikuwa akiwasilisha matokeo ya wiki tatu za utafiti jimboni Mwaro na Karusi ambapo tume hiyo iliwahoji watu 4,792 ambao walipoteza ndugu zao tangu migogoro ianze nchini humo.

    TRC imekuwa ikichunguza uhalifu wa wahusika wa mauaji yaliyotokea kati ya Julai 1, 1962 ambapo Burudi ilipata uhuru hadi Desemba 4, 2008 ambapo makubaliano ya kuacha mapigano yalisainiwa kati ya serikali ya Burundi na kundi la mwisho la waasi la FNL.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako