• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 61 wamekufa kutokana na tetemeko kubwa nchini Mexico.

    (GMT+08:00) 2017-09-09 18:21:11

    Tetemeko kubwa lenye kipimo cha Richter 8.2 limetokea pwani ya kusini nchini Mexico Alhamisi usiku na kusababisha vifo vya watu 61. Inaelezwa kuwa tetemeko hilo kubwa limesababisha uharibifu wa makazi mjini Mexico City, ambapo watu walikimbia kutoka katika majengo yao na kukimbilia mitaani.

    Wakati akihutubia taifa kupitia kituo cha televisheni, Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema jumla ya watu 61 wamekufa, watu 45 katika jimbo la Oaxaca, watu 12 jimbo la Chiapas na 4 Tobasco. Amekitaka kituo cha taifa cha kuzuia maafa kuendelea na shughuli za kutoa misaada ikiwemo maji na chakula na matibabu kwa majeruhi, na kusisitiza kuwa serikali itawasaidia wananchi kujenga upya makazi yao. Na ametangaza siku tatu za maombolezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako