• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia yaitaka Qatar iwe na udhati kwenye kutatua mgogoro

    (GMT+08:00) 2017-09-11 10:11:35

    Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Bw. Adel al-Jubeir tarehe 10 aliitaka Qatar iwe na udhati kwenye kutatua mgogoro, la sivyo Saudi Arabia itaendelea kuiwekea vikwazo.

    Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov, Bw. Jubeir amesema kuwa Qatar inajua nini cha kufanya.

    Ameitaka Qatar ithibitishe kwa dhati msimamo wake na kutatua mgogoro kati yao, hatua ambayo itasaidia kutekeleza kihalisi makubaliano yaliyofikiwa na pande zote. Makubaliano hayo ni pamoja na kusimamisha vitendo vya kufadhili ugaidi, kueneza chuki na kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.

    Bw. Lavrov pia amesema Russia inaunga mkono mgogoro wa Qatar utatuliwe kwa njia ya mazungumzo ya moja kwa moja, hivyo pande zote zinaweza kutoa maoni yao na kutafuta njia ya kutatua mgogoro huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako