• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wawili waliokamatwa Ufaransa wafanyiwa uchunguzi kuhusu kuwa na uhusiano na IS

    (GMT+08:00) 2017-09-11 10:15:07

    Mwendesha mashitaka wa Paris, Bw. Francois Molins amesema, wanaume wawili waliokamatwa wiki hii kwa kumiliki milipuko wanafanyiwa uchunguzi rasmi kujua kama wanahusika na ugaidi.

    Bw. Molins amesema watu hao walipanga kutengeneza bomu na kufanya shambulizi, lakini bado haijathibitishwa licha ya kuwa mmoja wao alikiri kwamba walikuwa wanapanga kuwashambulia askari wa operesheni ya Sentinel. Amesema walikubaliana kufanya shambulizi la kulipiza kisasi dhidi ya vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani.

    Ofisa huyo pia amedokeza kuwa, vifaa hivyo vya kutengeneza mabomu vilikamatwa katika operesheni ya kupambana na ugaidi iliyofanyika pembezoni mwa mji wa Paris.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako