• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kazi ya kurahisisha utaratibu wa kutoa idhini za serikali nchini China yaendelea

    (GMT+08:00) 2017-09-11 17:45:58

    Ofisa wa kikundi cha utekelezaji wa mageuzi ya utaratibu wa kutoa idhini cha baraza la serikali ya China amesema, tangu mwaka 2013 serikali ya China imeondoa taratibu karibu elfu moja za kutoa idhini za idara za baraza la serikali ili kupunguza mzigo kwa makampuni na wananchi. Katika siku za baadaye, serikali ya China itazidi kurahisisha utaratibu huo, na kuchochea shughuli za kiuchumi.

    Mhusika wa kikundi cha utekelezaji wa mageuzi ya utaratibu wa kutoa idhini cha baraza la serikali ya China Bw. Wu Zhilun amesema, hatua mpya zitachukuliwa katika kazi ya kurahisisha utaratibu wa kutoa idhini. Baraza la serikali ya China limeamua kueneza uzoefu wa mageuzi ya "Kutenganisha Kibali na Leseni" katika eneo jipya la Pudong la mji wa Shanghai, maeneo mengine 10 ya biashara huria huko Tianjin, Liaoning, Zhejiang na Fujian, kwa kufuta taratibu 52 za idara za baraza hilo na taratibu 22 za utoaji wa vibali za serikali za kimikoa. Mageuzi ya "Kutenganisha Kibali na Leseni" yanayaruhusu makampuni kupata leseni za kibiashara kabla ya kupata kibali maalumu cha utengenezaji na uuzaji, na kupunguza mzigo kwa mashirika na wananchi na kuzidi kuwarahisisha utaratibu. Bw. Wu amesema,

    "Bila kujali kama ni taratibu 52 za baraza la serikali, ama ni taratibu za serikali za kimikoa, mageuzi ya duru hiyo yanazitaka idara husika kutunga hatua halisi za kuimarisha usimamizi wa katikati na baada ya shughuli za kibiashara ndani ya siku 20 za kikazi. Kuondoa taratibu hizo kunalenga kupunguza vigezo vya makampuni kuingia katika shughuli hizo, lakini hakumaanishi serikali imeacha usimamizi, hivyo serikali itaimarisha usimamizi kwenye hatua za katikati na baada ya kuanza shughuli."

    Kuimarisha mageuzi ya utaratibu wa kutoa idhini na kuharakisha mageuzi ya uwezo wa serikali, ni mageuzi muhimu yaliyofanywa katika miaka ya hivi karibuni nchini China. Idara za serikali zimeimarisha nguvu ya usimamizi na kutoa huduma nyingi zaidi kwa kuhimiza ushindani wa usawa kwenye soko. Imefahamika kuwa tangu mwaka 2013, taratibu zaidi ya elfu moja zimeondolewa nchini China. Kwa mujibu wa ripoti kuhusu mazingira ya kibiashara ya dunia ya mwaka 2017 iliyotolewa na Benki ya Dunia, nafasi ya urahisi wa uendeshaji wa biashara nchini China imepanda na kufika 18. Bw. Wu amesisitiza kuwa mageuzi ya utaratibu wa kutoa idhini, hauna maana ya kupunguza vigezo tu, bali pia kutatoa huduma nzuri.

    "Jambo ambalo ni tofauti na zamani ni kwamba, mageuzi hayo hayasisitizi kurahisisha, bali pia yanasisitiza kuimarisha usimamizi na kuboresha huduma wakati kukurahisisha utaratibu. Kusema wazi, sio tu tutaondoa vikwazo vinavyozuia uendeshaji wa makampuni na kujiajiri kwa raia, bali pia tutaimarisha usimamizi ili kuepusha vurugu kutokea kwenye soko. Wakati huohuo, serikali pia itatoa huduma bora. Tunatilia maanani katika pande zote tatu. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako