• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Viwango vya riba vimewanyima wafanyibiashara wadogo na wa kati mikopo

  (GMT+08:00) 2017-09-11 20:32:09

  Biashara ndogo na za kati ndio waathiriwa wa kubwa na kuanzishwa kwa sheria ya kupunguza viwango vya riba, huku benki nyingi sasa zinadinda kuwapa mikopo.

  Kulingana na ripoti mpya ya utafiti wa mikopo iliyotolewa na Benki Kuu, zaidi ya nusu ya benki za Kenya hazipeani mikopo kwa wafanyibiashara wadogo.

  Ripoti hiyo inaonyesha kwamba asilimia 54 ya taasisi za fedha 42 ilipunguza mikopo yao kwa Biashara ndogo na za kati.

  Inaendlea kuonyesha kwamba asilimia 10 pekee ya taasisi za kifedha iliongeza utoaji wa mkopo kutokana na kiwango cha riba.

  Kati ya taasisi 42, asilimia 50 zinaonyesha kwamba mahitaji ya mkopo hayakubadilishwa wakati asilimia 15 ilibainisha kuwa mahitaji ya mkopo yalipungua kutokana na kuanzishwa kwa viwango vya riba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako