• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya asema nchi ni tulivu kufuatia ushindani wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2017-09-12 09:18:36

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewahakikishia viongozi wa wafanyabiashara kuwa nchi yake ni tulivu na hakuna atakayeruhusiwa kuvuruga amani.

    Rais Kenyatta aliyekuwa na mkutano na Muungano wa Sekta Binafsi KEPSA, ambao ni shirikisho la viongozi wa wafanyabiashara, amesema watendaji na mahakama wanafanya kazi wakati bunge linafunguliwa leo na mchakato wa kutunga sheria utaendelea. Amewaambia viongozi wa wafanyabiashara kupuuza kelele za kisiasa, na kuendelea na mipango ya kupanua ukuaji pamoja na kutoa ajira kwa vijana.

    Mkurugenzi Mkuu wa KEPSA Carole Kariuki amempongeza Rais Kenyatta kwa ahadi yake ya kulinda amani na kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara hata katika kipindi cha uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako