• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Tanzania laidhinisha mradi wa bomba la mafuta na Uganda

    (GMT+08:00) 2017-09-12 09:31:25

    Bunge la Tanzania limeidhinisha makubaliano kati ya serikali za Tanzania na Uganda kuhusu mradi wa bomba la mafuta.

    Bunge hilo limeidhinisha makubaliano hayo baada ya nchi hizo mbili kukubaliana kujenga bomba lenye urefu wa kilometa 1,445 kutoka kwenye eneo la mafuta huko Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

    Waziri wa sheria na katiba wa Tanzania Bw. Palamagamba Kabudi aliliambia bunge la nchi hiyo kuwa, Tanzania itanufaika kwa kupata dola za kimarekani bilioni 3.5 kutokana na mradi huo. Mbali na hayo, mradi huo unatarajiwa kutoa nafasi 10,000 za ajira wakati wa ujenzi, na nafasi nyingine 10,000 za ajira wakati wa utekelezaji wa mradi huo. Pia amesema mradi huo utawasaidia watanzania kupata uzoefu wa kuendesha miradi ya gesi na mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako