• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yamwita mwanadiplomasia wa Marekani kutokana na vikwazo

    (GMT+08:00) 2017-09-12 10:20:02

    Sudan Kusini imemwita mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani kupinga vikwazo ilivyowekewa hivi karibuni dhidi ya maofisa waandamizi wa serikali wa zamani na wa sasa.

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Bw. Bak Valentino Akol amesema, wamekutana na balozi mdogo wa ubalozi wa Marekani huko Juba Bw. Michael Morrow ili aeleze sababu za vikwazo hivyo ambavyo ameviita sio vya haki, wakati wanachama wa kundi la upinzani wakipuuzwa.

    Wizara ya fedha ya Marekani imeweka vikwazo na marufuku ya kusafiri ambavyo ni pamoja na kuzuia mali za waziri wa habari Bw. Micheal Makuei, Naibu mnadhimu mkuu wa jeshi la Sudan Kusini SPLA Bw. Reuben Malak na mkuu wa zamani wa jeshi hilo Bw. Paul Malong.

    Bw. Akol ameongeza kuwa huu ni uamuzi usio wa haki, kwa kuwa unawalenga watu wa upande wa serikali huku, ukiwaacha watu kutoka kundi la upinzani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako