• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la nishati ya atomiki duniani lasifu jitihada na mafankio ya China katika kuhakikisha usalama wa nyukilia

  (GMT+08:00) 2017-09-12 16:56:53

  Shirika la nishati ya atomiki duniani hivi karibuni limekamilisha tathmini kuhusu uhakikisho wa usalama wa nyuklia nchini China. Shirika hilo limeipongeza serikali ya China kwa jitihada zake za kuimarisha usalama wa nyukilia, na mafanikio ya China katika kuhakikisha maendeleo endelevu ya viwanda vya kinyukilia, na kushiriki kwenye uwekaji wa mfumo wa usimamizi kuhusu usalama na ulinzi wa nyukilia duniani.

  Mkurugenzi wa kituo cha usalama na ulinzi wa nyukilia cha China Bw. Deng Ge amesema, kwenye tathmini ilifanyika kuanzia tarehe 28 mwezi Agosti hadi tarehe 8 mwezi Septemba, kikundi cha tathmini kilichoundwa na wataalamu wanane kilitathmini mfumo wa usalama na ulinzi wa nyukilia nchini China na ulinzi wa vifaa vya nyukilia.

  Ripoti iliyotolewa na shirika la nishati ya atomiki duniani inasema, hivi sasa China imetangaza mpango wa maendeleo ya nishati ya nyukilia na vinu vya nyukilia, sekta ya nishati ya nyukilia na mfumo wa mzunguko wa nishati ya nyukilia utapata maendeleo ya kasi, hii imeleta changamoto mpya kwa utaratibu na usimamizi wa usalama na ulinzi wa nyukilia nchini China. Shirika la nishati ya atomiki duniani limependekeza China ikamilishe mapema kanuni na sheria za usalama na ulinzi wa nyukilia, kuharakisha mchakato wa utungaji wa sheria, na kuweka msingi imara wa kisheria kwa kazi ya usalama na ulinzi wa nyukilia.

  Bw. Deng Ge amesema serikali ya China siku zote inatilia maanani kazi ya usalama na ulinzi wa nyukilia, na inasimamia ipasavyo zana za nyukilia. Bw. Deng Ge amesema, kuhusu zana mpya zitakazojengwa, serikali ya China imeitaka sekta ya viwanda vya nyukilia ijenge mfumo wa usalama na ulinzi kwa mujibu wa vigezo vipya vya kimataifa, na juu ya vifaa vya zamani, serikali ya China imetoa mabilioni katika kuboresha mfumo wa uhakikisho wa nyukilia.

  Bw. Deng Ge amesema, kwa kupitia tathmini hiyo, China imeonesha sura ya nchi kubwa inayowajibika, na jumuiya ya kimataifa pia inaweza kuelewa zaidi maendeleo ya viwanda vya nyukilia nchini China. Nchi nyingine zitakuwa na imani zaidi kuhusu umeme unaozalishwa kwa nishati ya nyukilia nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako