• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wabunge watahadharisha kuhusu ulipaji wa fidia maeneo ya mradi wa ujenzi wa bomba

  (GMT+08:00) 2017-09-12 18:51:40

  Wabunge wa Tanzania wameitahadharisha Serikali kuhusu ulipaji wa fidia maeneo ambayo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga litakapopita, huku wapinzani wakisema mkataba wa mradi huo unakinzana na sheria za nchi.

  Waliyasema hayo bungeni Jumatatu wakati wakichangia azimio la kuridhia mkataba baina ya Serikali na Uganda, kuhusu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

  Mbunge wa Tanga Mjini (CUF), Mussa Mbarouk alitoa mfano wa eneo la Chongoleani ambako wananchi wamelipwa fidia ya Sh2 milioni kwa eka, baadhi walitaka ufafanuzi sababu ya kulipwa kiwango hicho ilhali wapo walionunua kwa zaidi ya Sh10 milioni.

  Akijibu hoja hizo , Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema Sheria iliyopitishwa na Bunge inahusiana na Maliasili na Rasilimali za Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako