• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia latwaa udhibiti wa mji wa mpakani baada ya mapambano makali

    (GMT+08:00) 2017-09-12 18:58:36

    Jeshi la serikali ya Somalia limetwaa udhibiti wa mji wa Bulla Hawa ulio kwenye mpaka na Kenya, baada ya mapambano ya makali na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.

    Wapiganaji wa kundi la Al Shabaab walivamia kambi ya jeshi ya mji wa Bulla Hawa baada ya kufanya shambulizi la mlipuko wa gari, na kusema limewaua wanajeshi 24 wa jeshi la serikali ya Somalia. Wenyeji wamesema wapiganaji hao walivamia kituo cha jeshi na kituo cha polisi. Baadaye waliharibu majengo ya serikali na kupora maduka wakati wakikimbia.

    Kwenye shambulizi hilo wanajeshi 180 wa jeshi la Somalia walivuka mpaka na kuingia mjini Mandera nchini Kenya wakiwakimbia wapiganaji hao. Jeshi la Kenya limethibitisha kuwa limewasindikiza wanajeshi hao mjini Bulla baada ya ndege zake kuwashambulia vikali wapiganaji wa Al Shabaab, na sasa jeshi la serikali ya Somalia linaushikilia mji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako