• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa ulinzi wa Russia akutana na rais wa Syria

  (GMT+08:00) 2017-09-13 09:27:22

  Waziri wa ulinzi wa Russia Bw. Sergei Shoigu amekutana na rais Bashar al-Assad wa Syria, na kufikisha salamu za pongezi za rais Vladimir Putin kutokana na maendeleo yaliyopatikana katika kuukomboa mji wa Deir ez Zor. Viongozi hao pia wamezungumzia ushirikiano kati ya majeshi ya Syria na Russia kuendelea na operesheni za kuukomboa kikamilifu mji wa Deir ez Zor kutoka kwa magaidi. Shirika la habari la Syria SANA limesema Russia imetuma wahandisi 157 kusaidia kuondoa mabomu ya ardhini, yaliyotegwa na kundi la Islamic State kwenye eneo la Deir ez Zor.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako