Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Sudan amesema kwenye taarifa yake kuwa, Bw. Ghandour pia ataongoza ujumbe wa Sudan kuhudhuria Mkutano wa 72 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson na maofisa wengine waandamizi.
Mwishoni mwa mwezi Julai, Marekani ilirefusha kwa miezi mitatu muda wa kupitia uamuzi wake kama itaondoa kabisa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Sudan vilivyowekwa kutokana na rekodi ya haki za binadamu ya nchi hiyo na masuala mengine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |