• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 72 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wafunguliwa

  (GMT+08:00) 2017-09-13 10:18:36

  Mkutano wa 72 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umeanza rasmi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Kuzingatia maslahi ya watu: Kujenga amani na maisha bora kwa binadamu wote katika dunia yenye maendeleo endelevu".

  Mwenyekiti wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajcak, amesema baraza hilo litafanya juhudi katika sekta tatu zikiwemo kuzingatia maslahi ya watu, kusawazisha maslahi ya pande mbalimbali na kuongeza ufanisi na uwazi wa kazi. Pia amesisitiza kuwa inapaswa kuzidisha mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

  Pia ameitaka China iendelee kutoa mchango muhimu katika mambo ya kimataifa, na kuwa kiongozi katika masuala ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako