• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Korea Kaskazini yapinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2017-09-13 19:00:05

  Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imelaani vikali azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu nchi hiyo, na kusema "limekwenda kinyume cha sheria".

  Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, Marekani imechukua hatua isiyofaa kupitisha azimio hilo namba 2375 ambalo linalenga kuondoa haki ya Korea Kaskazini ya kujilinda. Pia taarifa hiyo imesema Korea Kaskazini itaendelea kulinda haki yake na kuharakisha kuongeza nguvu zake za kijeshi.

  Habari zinasema, Baraza la Usalama jana limepitisha azimio hilo na kuamua kuweka vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako