• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Shirika la Afya ya Mazao laongeza kasi ya vita dhidi ya mbegu feki

  (GMT+08:00) 2017-09-13 19:07:34

  Shirika la ukaguzi wa afya ya mazao nchini Kenya (Kephis) limezindua huduma ya ujumbe mfupi ili kuwalinda wakulima dhidi ya mbegu feki.

  Mkurugenzi wa Kephis Esther Kimani amesema hatua hiyo inalenga kuwaondoa sokoni wafanyabiashara wanaouza mbegu zisizopimwa ambazo hufanya vibaya na kusababisha wakulima kupata hasara.

  Alisema wafanyabisahra hao ndio wanaosababisha uhaba wa chakula nchini na kuifanya nchi ya Kenya kutumia mabilioni ya pesa kuagiza chakula kutoka nje kila mwaka.

  Bi Kimani alisema huduma hii m pya ya usalam inawalenga wakulima wadogo ambao wananunua pakitia za kati ya kilo moja hadi tano za mbegu.

  Huduma hii mpya itawawezesha wakulima kugundua iwapo mbegu ni feki kwa kukwaruza muhuri ulioko kwenye pakiti ili kuona nambari halafu kuzituma nambari hizo kwa 1393 kwa njia ya ujumbe mfupi kutumia simu.Baadaye atapokea ujumbe kutoka Kephis utakaothibitisha kama mbegu hizo ni halisi au feki.

  Huduma hiyo inajumuisha mazao yote yanayouzwa na kampuni za ndani katika Jumiya ya Afrika Mashariki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako