• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Kampuni ya Namera kununua pamba yote itakayiozalishwa nchini Tanzania

  (GMT+08:00) 2017-09-13 19:08:15

  Kampuni ya Namera Group of Industries nchini Tanzania imeahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini humo kuanzia msimu ujao.

  Ahadi hii ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Namera Group of Industries Bw Hamza Rafiq Pardesi alipokutana na kufanya mazungumzo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenya makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali tayari imeanza kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

  Waziri Mkuu amempongeza Bw Pardesi kuiunga mkono serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi na kupitia sekta ya viwanda.Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kmapuni hiyo inatarajia kufunguya kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.

  Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbele alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba mwishoni mwa wiki iliyopita na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.

  Waziri Mkuu amesema serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba,kupanda,matumizi ya pembejeo na dawa,kuvuna na kutafuta masoko ,hivyo ahadi ya kampuni ya Namera ya kununua pamba yote ni faraja kwa wakulima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako