• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasaidia Uganda kuendeleza sekta ya afya

    (GMT+08:00) 2017-09-14 10:06:53

    Waziri wa afya wa Uganda Bibi Ruth Aceng amesema China imeipatia Uganda misaada mingi kwenye maendeleo ya sekta ya afya.

    Bibi Ruth jana alihudhuria na kuhutubia hafla ya kukaribisha kikundi kipya cha madaktari wa China katika Hospitali ya Urafiki kati ya China na Uganda mjini Kampala, na kuishukuru serikali ya China kwa kuendeleza ushirikiano na Uganda na kutuma madaktari nchini humo.

    Kikundi hicho chenye madaktari tisa wa China kitafanya kazi kwa miaka miwili kwenye hospitali hiyo iliyojengwa na China mwaka 2012, na kuwapatia wananchi wa Uganda matibabu bila malipo.

    Balozi wa China nchini Uganda Bw Zheng Zhuqiang amesema kutumwa kwa kikundi cha madaktari wa China nchini Uganda ni njia kuu kwenye sekta ya ushirikiano wa huduma za afya kati ya China na nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako