• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanafunzi wengi zaidi wa Afrika watafuta elimu bora nchini China

  (GMT+08:00) 2017-09-14 10:54:19

  Balozi wa China nchini Zambia Bw. Yang Youming amesema, ongezeko la idadi ya wanafunzi wa Afrika wanaokuja kusoma China ni alama wazi ya elimu bora inayotolewa nchini China.

  Bw. Yang amesema China inafurahi kuona mfumo wa elimu yake unapendwa na nchi za Afrika, na imeahidi kuendelea kutoa elimu bora.

  Bw. Yang ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari ambako alitangaza barua 11 za shukrani kati ya wanafunzi 26 waliokuja China mwaka jana kwenye mafunzo ya usanii chini ya mpango ulioandaliwa na mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan na mwenzake wa Zambia Bibi Esther Lungu.

  Bw. Yang ameongeza kuwa China imekuwa nchi inayochaguliwa sio tu na vijana wa Zambia wanaotaka kusoma nje, bali pia kwa Afrika nzima, huku akisema China imekuwa nchi ya pili inayowavutia wanafunzi wengi zaidi wa Afrika baada ya Ufaransa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako