• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari ya Mombasa yapitisha asilimia 11.9 zaidi ya bidhaa katika miezi 7 ya mwaka huu.

    (GMT+08:00) 2017-09-14 16:37:36

    Takwimu zilizotolewa na idara ya mambo ya bandari ya Kenya zimeonyesha kuwa, idadi ya bidhaa zilizopita kwenye bandari ya Mombasa katika miezi 7 ya mwanzo ya mwaka huu imeongeza kwa asilimia 11.9 ikilinganishwa na mwaka jana.

    Idara hiyo imesema, katika kipindi hicho, bandari ya Mombasa imepitisha tani milioni 17.5 za bidhaa, na idadi ya kusafiri nje ya bandari hiyo imeongeza kwa asilimia 1.7.

    Habari zinasema, kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa reli ya SGR iliyojengwa na kampuni ya China, bandari hiyo inatarajia kupitisha bidhaa nyingi zaidi katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako