• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa huko wanufaika na chai ya Fulianggong

    (GMT+08:00) 2017-09-14 16:58:26

    Wilaya ya Fuliang iko kwenye sehemu ya kaskazini mashariki mkoani Jiangxi, China, na inafahamika kwa kuwa sehemu maarufu ya uzalishaji wa chai tangu zama za kale. Hivi sasa chai inayozozalishwa na kampuni ya chai ya Fulianggong, si kama tu imehimiza maendeleo ya sekta ya chai ya wilaya hiyo, bali pia zimesaidia wakazi wa huko kujiongezea mapato.

    Fulianggong ni chapa iliyoanzishwa mwaka 2006 na Mzee Ji Xiaoqing na familia yake. Mwaka ule Bw. Ji aliyekuwa na umri wa miaka 50 alistaafu kwa mujibu wa marekebisho ya utaratibu wa kazi. Aliamua kutumia uzoefu wake kwenye kituo cha sayansi ya kilimo, na kujihusisha na kilimo cha kisasa.

    Kutokana na msaada wa chuo cha kilimo cha chuo kikuu cha Zhejiang, mwanzoni Bw. Ji alichagua kukuza chai isiyo na uchafuzi. Hivi sasa shamba lake la chai lenye eneo la kilomita 2 za mraba limethibitishwa na wizara ya uhifadhi wa mazingira ya China kuwa kituo cha msingi kinachozalisha vyakula visivyo na uchafuzi, na chai yake pia imepata kibali cha mazao yasiyo na uchafuzi cha Umoja wa Ulaya.

    Bw. Ji amesema, mwaka 2007 alipojenga kiwanda cha kwanza, aliuza nyumba yake. Wakati ule mke wake hakukubali, na alikuwa analia mara kwa mara, kwani nyumba hiyo ilikuwa ndio nyumba yao kubwa, lakini Bw. Ji alishikilia kuiuza. Baada ya kujenga kiwanda, kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuzalisha chai, Bw. Ji aliuza nyumba nyingine.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya chai ya kaunti ya Fuliang Bw. Xu Zhaoming amesema, wakulima wa huko waliofanya kazi mjini ni wachache, kwani mashamba ya chai ikiwemo shamba la chai la Fulianggong yametoa nafasi nyingi za ajira, na wakulima wa huko wamekuwa na njia mpya ya kupata mapato.

    Bw. Xu Zhaoming amesema, kampuni ya Fuliangong kila mwaka inaajiri wafanyakazi zaidi ya 100, hasa katika majira ya kuchuma chai, inahitaji kuajiri wafanyakazi zaidi ya mia tatu. Katika majira ya kuchuma chai, kampuni ya Fulianggong huajiri watu wenye ulemavu, na kuwapa malipo sawa na watu wengine wa kawaida.

    Bw. Ji ana wasiwasi kuhusu maendeleo ya shamba la chai katika siku za baadaye. Anaona kuwa maendeleo ya chai yanategemea watu wenye ujuzi, lakini hivi sasa vijana wenye ujuzi huu ni wachache. Hivyo Bw. Ji ameandaa watu wenye ujuzi wa chai kupitia kuwasaidia wanafunzi kutoka familia zenye matatizo kiuchumi.

    Bw. Ji amesema mwanafunzi mmoja anayemsaidia atahitimu kutoka chuo cha chai ya Wuyuan mwaka kesho. Familia yake ni maskini, na kampuni ya Fulianggong ilitoa msaada wa kiuchumi kwake wakati walipoingia chuo kikuu. Mwanafunzi huyo alisomea ujuzi wa mfumo wa sifa za chai na utaraibu wa uzalishaji wa chai.

    Kutokana na takwimu zilizotolewa na idara ya chai ya kaunti ya Fuliang, wakulima elfu 55 wanajishughulisha na mambo ya chai, na kila mtu anapata yuan 8300 kwa mwaka. Bw. Ji anatumai kurithisha historia ya chai na kuwanufaisha wakulima wa huko kupitia juhudi zake, hasa juhudi za vijana wa kaunti ya Fuliang waliopata elimu ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako