• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: BancABC yaanzisha akaunti mpya isiyo na gharama

    (GMT+08:00) 2017-09-14 18:58:29

    Benki ya BancABC nchini Tanzania imezindua akaunti iitwayo Jiongeze Hundi inayolenga kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali kufanya miamala bila kutumia gharama kubwa.

    Akaunti hiyo inapunguza makato ya huduma za uendeshaji wa akaunti ya kila mwezi kwa wateja watakaoifungua.

    Meneja wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Joyce Malai amesema akaunti ya Jiongeze inaweza kuwa ya biashara au ya mshahara lakini haitakatwa gharama kubwa za mwezi kwa muda wa mwaka mmoja tangu ifunguliwe.

    Malai amesema faida zingine kwa wateja wa Jiongeze ni kuangalia salio sehemu yoyote kupitia simu ya mkononi, kuweka na kutoa fedha kupitia zaidi ya mawakala 50 ambao wanapatikana sehemu mbalimbali za Dar es Salaam, kupitia mtandaoni na ATM zenye nembo ya visa.

    BancABC mwaka huu imeshinda tuzo ya benki inayokua kwa haraka.

    Amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali kufungua akaunti ya Hundi ya Jiongeze kwa kuwa huduma hiyo itadumu kwa miezi miwili pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako