• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mganda Emmanuel Okwi atangazwa mchezaji bora wa mwezi August wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:46:02

    Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea club ya Simba SC ya Tanzania Emmanuel Okwi jana alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi August wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara.

    Okwi ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kuwashinda kiungo wa Mtibwa Sugar Mohammed Issa aliyesaidia timu yake kupata pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United na Boniface Maganga wa Mbao FC.

    Mchezaji huyo alifanikiwa kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kamati ya tuzo ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako