• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 83 wauawa na wengine 93 wajeruhiwa katika mashambulizi mawili kusini mwa Iraq

    (GMT+08:00) 2017-09-15 09:56:36

    Watu zaidi ya 83 wameuawa na wengine 93 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya bomu lililotegwa kwenye gari na ufyatuaji risasi karibu na mji wa Nasriyah kusini mwa Iraq.

    Mkuu wa idara ya afya ya mkoa wa Dhi Qar Bw. Jasim al-Khaledi amesema, idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari na mashambulizi katika eneo la Fadak imeongezeka hadi 83 na wengine 93 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa katika hali mbaya.

    Bw. Khaledi amesema, vifo na majeruhi hao ni pamoja na raia wengi wa Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako