• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar es Salaam-Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imepunguza hasara kwa kiasi kikubwa kutoka Sh bilioni 20 hadi kufi kia Sh bilioni 3 kwa mwaka.

    (GMT+08:00) 2017-09-15 18:13:00

    Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Ladislaus Matindi amesema katika mpango wao wa muda mfupi ambao ni wa mwaka mmoja, wamefanikiwa kupunguza hasara kwa kiasi hicho. Matindi amesema kufanikiwa huko kumetokana na kufanyika kazi katika baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa ni changamoto ikiwemo ufutaji wa safari, akieleza kuwa awali walikuwa wakifuta safari, lakini kwa sasa hawafuti safari.

    Pia kumekuwapo na udhibiti wa mapato. Amesema wamejiwekea Mpango Mkakati wa Biashara wa muda mrefu ambao ni wa miaka mitano na kwamba una malengo matatu ikiwemo usalama, kuhakikisha wanatengeneza faida pamoja na kutoa huduma zenye uhakika kwa wateja wao. Aidha, alisema wamejiwekea tathmini ikiwa ni pamoja na kuangalia mambo ambayo ni hatari na jinsi ya kukabiliana nayo.

    ATCL kwa sasa inamiliki ndege mbili aina ya Bombardier Q400 zinazotoa huduma katika sehemu mbalimbali nchini ambazo zimenunuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kulirejesha shirika hilo katika usafiri wa anga. Ndege nyingine inatarajiwa baadaye mwaka huu. Naye Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la ATCL, Margret Leslie amesema lengo la kuwepo kwa baraza hilo ni kuwakutanisha wafanyakazi na menejimenti ili kupanga maendeleo na matarajio yao ya baadaye

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako