• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama lalaani vikali kufanya jaribio la kurusha makombora tena kwa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-16 18:13:26

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana lilitoa taarifa likilaani vikali kufanya jaribio la kurusha makombora tena kwa Korea Kaskazini na likieleza kuwa hiki ni kitendo cha uchochezi dhidi ya jumuiya ya kimataifa.

    Kutokana na maombi ya ujumbe wa Marekani na Japan wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa, baraza la usalama ijumaa alasiri lilifanya majadiliano kuhusu jaribio la kurusha makombora la Korea Kaskazini, baada ya majadiliano hayo baraza la usalama liliilaani vikali na kuionya Korea Kaskazini isimamishe vitendo vyote kama hicho mara moja.

    Taarifa hiyo ilionesha kuwa, baraza la usalama linaona hivi karibuni vitendo na kauli za Korea Kaskazini zinaharibu amani na utulivu wa kikanda na kuleta wasiwasi mkubwa kwa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako