• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Al-Shabaab yatwaa sehemu ya mpaka na Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-17 18:27:19

    Kikundi cha Al-Shabaab wenye silaha kali Jumamosi asubuhi walivamia kambi ya jeshi la taifa la Somalia (SNA) huko Bula Hache, kilomita chache kutoka mjini Elwak karibu na mpaka wa Somalia na Kenya.

    Maafisa wa Kenya na Somalia walisema wapiganaji waliutwaa mji huo kabla ya kuondoka baada ya mapigano makali yaliyoanza Ijumaa usiku na kumalizika Jumamosi asubuhi.

    Kwa mujibu wa Naibu kamishna wa kaunti, Daniel Bundotich alisema wapiganaji walifika katika kambi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kabla ya kuchoma moto mali na silaha za jeshi la taifa la Somalia na kueleza kuwa kikosi cha ulinzi cha Kenya (KDF) kilitumia makombora ya kwenye ndege kukomboa kambi hiyo kutoka kwa wapiganaji hao.

    Shambulio la karibuni limekuja baada ya Al-Shabaab kuvamia kambi ya polisi iliyopo Bula Hawa karibu na mji wa Mandera siku ya jumatatu kabla ya vikosi vya usalama vya Kenya kurejesha toka kwa wapiganaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako