• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uingereza yashusha ngazi ya tishio la kigaidi

  (GMT+08:00) 2017-09-18 09:21:46

  Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Bibi Amber Rudd amesema ngazi ya hatari ya tishio la shambulizi nchini humo imepunguzwa, baada ya kutajwa kuwa ya juu kabisa kufuatia mlipuko uliotokea kwenye kituo cha subway.

  Taarifa iliyotolewa na polisi wa Uingereza inasema watu wawili, mmoja akiwa na umri wa miaka 18 na mwingine akiwa na miaka 21, walikamatwa jumamosi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.

  Jumla ya watu 30 walijeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea kwenye behewa la subway ijumaa iliyopita mjini London, na kuwalazimu polisi kuanza msako mkubwa dhidi ya wahusika.

  Kundi la IS limetangaza kuhusika shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako