• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Ecobank Tanzania yaanzisha huduma ya malipo mtandaoni

    (GMT+08:00) 2017-09-18 18:09:54

    Benki ya Ecobank imeanzisha kwa mara ya kwanza huduma ya malipo mtandaoni yanayohusu viza na Mastercard bila kutumia kadi kupitia programu ya simu.

    Uanzishwaji wa huduma hiyo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wengi zaidi na kuwarahisishia kufanya biashara kwa kuwaruhusu kufanya miamala katika maeneo tofauti duniani.

    Mkurugenzi mpya wa Ecobank, Mwanahiba Mzee amesema jana Alhamisi kuwa, huduma hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo itakuwa sehemu ya uboreshaji wa programu ya sasa ya Ecobank mobile app ambayo inarahisisha ufanyaji miamala kutoka na kwenda benki na akaunti za fedha za simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako